COVID-19 (virusi vipya vya korona) – Maelezo, huduma, na nyenzo katika Jimbo la Washington

Nambari ya Simu ya COVID-19: Msaada kwa wafanyakazi, biashara, miadi ya chanjo na zaidi

Iwapo una maswali kuhusu COVID-19 au unahitaji msaada wa kupata miadi ya chanjo, tafadhali piga simu kwa 1-800-525-0127 na ubonyeze #. Watakapojibu, taja lugha yako ili upate huduma za ukalimani. Nambari hiyo ya simu iko wazi kila siku saa zake zimeorodheshwa katika tovuti ya Department of Health (katika Kiingereza pekee).

Ripoti ukiukaji wa kibiashara

Biashara zinapaswa kuchukua hatua zinazofaa za afya na usalama kwa ajili ya wafanyakazi na wateja. Iwapo unataka kuripoti ukiukaji, tafadhali piga nambari ya simu ya COVID-19 iliyo hapo juu ili kupata msaada katika lugha yako. Mtu fulani atakuuliza maswali kuhusu ukiukaji huo na kuwasilisha malalamishi kwa niaba yako. Hutahitajika kupeana jina lako au habari zako za mawasiliano ili kuwasilisha malalamishi.

Unaweza pia kuwasilisha malalamishi katika Kiingereza kwenye ukurasa wa Ripoti Ukiukaji wa COVID-19.

Tafadhali zingatia kwamba ikiwa utatoa jina lako au habari yako za mawasiliano, zinaweza kufunuliwa ikiwa mtu atawasilisha ombi la rekodi za umma kwa ajili ya habari hizo. Rekodi zinazofafanuliwa katika Taarifa ya Faragha ya gavana (katika Kiingereza pekee) zitatolewa jinsi zinavyopaswa kulingana na Sheria ya jimbo ya Rekodi za Umma, RCW 42.56.

Msaada zaidi kwa wafanyakazi, biashara na mashirika

Kwa kutumia huduma za utafsiri, nambari hio ya simu inaweza kukuelekeza kwa mwongozo wa jumla na rasilimali. Zinaweza pia kukusaidia kujaza fomu ya COVID-19 ya Maswali ya Biashara na Wafanyakazi ikiwa bado una maswali. Utaombwa kuandaa habari za mawasiliano ili uweze kupata jibu.

Chanjo ya Virusi vya Korona (COVID-19)

Kwa maelezo zaidi kuhusu chanjo za COVID-19, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Chanjo dhidi ya COVID-19.

Programu ya simu mahiri ya arifa za kuwa katika hatari ya WA Notify
Image
JINSI PROGRAMU/KIPENGELE CHA WA NOTIFY HUFANYA KAZI

WA Notify (Arifa ya WA) (inayojulikana pia kama Washington Exposure Notifications (Taarifa za Mfiduo wa Washington) ni zana ya bila malipo inayofanya kazi kwenye simu mahiri kuwaarifu watumiaji iwapo huenda waliambukizwa COVID-19 bila kushiriki maelezo yoyote ya kibinafsi. Ni ya kibinafsi kabisa na haijui wewe ni nani au haifuatilii pahali unapoenda.

Ninaweza kuongeza vipi WA Notify kwenye simu yangu?

Kwenye iPhone, wezesha Exposure Notifications katika Mipangilio:

 • Nenda kwenye Mipangilio (Settings)
 • Telezesha chini hadi kwa Exposure Notifications
 • Bofya "Washa Exposure Notifications”
 • Teua United States (Marekani)
 • Teua Washington

Kwenye Android phone:

Kwenye Android au iPhone, tambaza msimbo wa QR:

WA Notify QR code

Inafanya kazi vipi?

Unapoamilisha WA Notify, simu yako hubadilisha misimbo nasibu isiyofahamika kwenye simu za watu ulio karibu nao ambao tayari wamewezeshwa WA Notify. Programu hiyo hutumia faragha inayohifadhi taknolojia ya Bluetooth ya Kawi ya Chini kubadilisha misimbo hii nasibu bila kutoa maelezo yoyote kukuhusu. Iwapo mtumiaji mwingine wa WA Notify ambaye umekuwa karibu naye katika wiki mbili baadaye atapatikana na maambukizo ya COVID-19 na anafuata hatua za kuwaarifu wengine bila kujitambulisha, utapata taarifa isiyotambulisha jina kuwa ulikuwa na mfiduo wenye uwezekano. Hatua hii itakusaidia kupata huduma unayohitaji kwa haraka na pia itakusaidia kujikinga na kusambaza COVID-19 kwa watu walio karibu nawe.

Algorathim hufanya hesabu ya kutambua matukio yanayoweza kusambaza COVID-19 kutoka kwa wale walio katika umbali salama au fupi ya kutosha ambayo huhitaji kuonywa. WA Notify itakuarifu tu ikiwa huenda umekuwa karibu na mtu aliyeambukizwa. Hivyo kutopokea arifa ni habari njema.

WA Notify inapatikana katika lugha zaidi ya 30 hivyo wakazi wengi wa Washington kadri inavyowezekana wanaweza kufikia zana hii.

Jinsi ya kuripoti matokeo yako ya kipimo cha nyumbani yanayoonyesha kuwa una maambukizo

Watu wanaonunua vifaa vya kipimo vya kununuliwa dukani na kupokea matokeo yanayoonyesha wana maambukizo wanafaa kupiga nambari ya simu ya COVID-19 ya jimbo, 1-800-525-0127 kisha kubonyeza # (bonyeza 7 kupata Kihispania), mara tu wanapopokea matokeo. Nambari hiyo ya simu inapatikana Jumatatu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku, na Jumanne hadi Jumapili (na sikukuu) saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Usaidizi wa lugha unapatikana.

Ukipiga simu, kuwa na uhakika ili kuwafahamisha kuwa wewe ni mtumiaji wa WA Notify (Arifa ya WA). Mfanyakazi wa nambari ya simu anaweza kukupatia kiungo cha uthibitisho unachoweza kutumia ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify kuwa huenda wamekuwa na mfiduo.

Tafadhali kumbuka: WA Notify ni zana ya taarifa ya mfiduo. Haikuundwa ili watumiaji waingize matokeo yao ya kipimo.

Faragha yangu inalindwa vipi?

WA Notify inategemea teknolojia ya Taarifa ya Mfiduo wa Google Apple, ambayo imeundwa ili kulinda faragha yako. Inafanya kazi kwenye mandharinyuma bila kukusanya au kufichua eneo lolote au data ya kibinafsi, na haihitaji kujua wewe ni nani au uko wapi ili kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa kutumia vidude hivi vidogo vya Bluetooth, betri yako haiathiriwi.

Ushiriki ni wa kujitolea. Mtumiaji anaweza kuingia au kujitoa wakati wowote. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi faragha ya mtumiaji inalindwa, tazama sera ya faragha ya WA Exposure Notifications.

Taarifa hukaa vipi?

Kuna aina mbili za taarifa unazoweza kupokea. Wanaopatikana na maambukizo watapokea ujumbe wa matini wenye kiungo cha uthibitishaji na/au taarifa ibukizi. Watumiaji wa WA Notify ambao huenda walikuwa na mfiduo watapokea taarifa ya mfiduo. Jifunze zaidi kuhusu taarifa hizi na uone zinavyokaa.

Itasaidia vipi?

Utafiti wa hivi karibuni wa University of Washington (Kiingereza pekee) ulipata kuwa watu wanavyozidi kutumia taarifa ya mfiduo, ndivyo manufaa yanakuwa makubwa. Matokeo yalionyesha kuwa WA Notify iliokoa karibu maisha 40-115 na huenda ikazuia karibu visa 5,500 vya COVID-19 wakati wa miezi minne ya kwanza ilipotumika. Mifumo ya data inaonyesha kuwa hata idadi ndogo ya watu wanaotumia WA Notify inaweza kupunguza maambukizo na vifo vya COVID-19, ikionyesha kuwa WA Notify ni zana bora ya kuzuia msambao wa COVID-19.

Unataka kusaidia kutangaza habari kuhusu WA Notify (Taarifa za WA)?

Angalia chombo cha zana WA Notify kwa ajili ya utumaji ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, mabango, sampuli ya matangao ya redio na televisheni, na zaidi.

Maswali mengine yanayoulizwa mara kwa mara

Nilipokea taarifa na/au matini kutoka kwa Washington State Department of Health (DOH, Idara ya Afya ya Jimbo la Washington). Kwa nini?

DOH hutuma ujumbe wa matini na/au taarifa ibukizi kwa kila mtu ambao hivi karibuni walipatikana na maambukizo ya COVID-19 ili watumiaji wa WA Notify waweze kuwaarifu watumiaji wengine kwa haraka na bila kujulikana kuhusu mfiduo. Jifunze zaidi kuhusu taarifa hizi na uone zinavyokaa.

Ukipokea zote mbili, unahitaji tu kudonoa taarifa au kubofya kwenye kiungo katika ujumbe wa matini na kufuata hatua katika WA Notify ili kuwaarifu watumiaji wengine bila kujulikana kuhusu mfiduo ambao huenda ulitokea.

Je, nahitaji WA Notify ikiwa nimepokea chanjo?

Ndiyo. Hata baada ya kupokea chanjo kamili dhidi ya COVID-19, bado unahitaji kutekeleza tahadhari za kawaida za janga hili. Chanjo ni njia faafu ya kujilinda, lakini bado kuna hatari kidogo kuwa unaweza kuambukizwa au kuwaambukiza wengine ambao hawajapewa chanjo.

Nilipata arifa kuhusu kuchangia data yangu ya WA Notify kwa afya ya umma. Kwa nini?

Washington State Department of Health (DOH) inataka kujua jinsi WA Notify inafanya kazi vizuri ili tuweze kufanya uboreshaji wowote unaohitajika kwenye zana hiyo. Ukikubali kushiriki data yako ya WA Notify, faragha yako bado inalindwa kamili. Hakuna maelezo ya kibinafsi yatakayokusanywa au kushirikiwa na hakuna njia ya kukutambua. DOH pekee ndiyo inaweza kufikia data hii na katika kiwango cha jimbo pekee.

Ikiwa watumiaji wa WA Notify watakubali kushiriki data yao, ni nini itakusanywa?

Ukikubali kushiriki data yako, faragha yako bado inalindwa kamili. Hakuna maelezo ya kibinafsi yatakayokusanywa au kushirikiwa hivyo hakuna njia ya kukutambua. Washington State Department of Health pekee ndiyo inaweza kuona data hii ya kiwango cha jimbo, itakayojumuisha:

 • Idadi ya watu wanaokubali kushiriki data yao kutoka WA Notify. Hii hutusaidia kujua jinsi sampuli yetu inawakilisha.
 • Idadi ya Exposure Notifications zilizopokelewa na watumiaji wa WA Notify. Hii hutusaidia kuona mwelekeo katika msambao wa COVID-19.
 • Idadi ya watu wanaobofya kwenye taarifa ya mfiduo. Hii hutusaidia kuchunguza jinsi watu wako tayari ili kuzingatia mapendekezo ya afya ya umma.

Idadi ya watu waliokuwa karibu na mtu aliyepatikana na maambukizo ya COVID-19, lakini si karibu ya kutosha au kwa muda wa kutosha kuarifiwa kuhusu mfiduo. Hii hutusaidia kuzingatia kama kanuni ambayo huamua mfiduo katika WA Notify inafaa kurekebishwa.

Nikiwezesha WA Notify kwenye iPhone yangu, nafaa kuwasha au kuzima togoa ya "Availability Alerts (Arifa za Upatikanaji)"?

Kuzima ni sawa. Ijapokuwa kuwasha kumependekezwa ikiwa unasafiri nje ya jimbo la Washington kwa kipindi kirefu cha muda. Arifa za Upatikanaji zikiwa zimewashwa, unaweza kupokea taarifa ukisafiri kwenda kwa eneo lenye teknolojia ya taarifa ya mfiduo tofauti na WA Notify. watumiaji wa iPhone wanaweza kuongeza maeneo kadhaa lakini kuteua eneo moja pekee kama amilifu kila mara. Huhitaji kuondoa eneo ili kuwezesha mpya. Watumiaji wa Android wanaweza kusakinisha programu za taarifa ya mfiduo kama WA Notify kutoka majimbo kadhaa lakini programu inayotumia teknolojia inayoendana na WA Notify ndiyo inawekwa amilifu kwa wakati.

Je, ni lazima niingie ili kutumia WA Notify?

Ndiyo. WA Notify ni ya bure na ya kujitolea. Unaweza kujiondoa wakati wowote. Zima tu kipengele hicho au futa programu hiyo. Misimbo yote nasibu ambayo simu imehifadhi kutoka kwa watumiaji wa karibu itafutwa na haiwezi kupatikana tena.

Je, WA Notify ni programu ya kufuatilia mwasilani?

La. WA Notify haifuatilii maelezo kuhusu watu ambao umekuwa karibu nao, hivyo "haifuatilii waasilani". Ufuatiliaji wa mwasilani hutambua mtu yeyote ambaye mtu aliyepatikana na maambukizo ya COVID-19 huenda amekuwa karibu naye. Programu hiyo haikusanyi au kubadilisha maelezo yoyote ya kibinafsi, hivyo haiwezekani kwa mtu yeyote kujua mwasilani wako.

"Mfiduo" ni nini?

Mfiduo hufanyika wakati umechukua muda wa kutosha karibu na mtumiaji mwingine wa WA Notify ambaye baadaye hupatikana na ugonjwa wa COVID-19. Hii hufuata mwongozo wa sasa kutoka Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) (Kiingereza pekee) kuhusu kukaa mbali na mwingine na kupitishwa kwa COVID-19. Ili kuamua mfiduo, WA Notify hutumia kanuni ambayo hulandanisha na ufafanuzi wa CDC wa mwasilani wa karibu - ndani ya karibu futi 6 (mita 2) kwa dakika 15 au zaidi wakati wa kipindi cha maambukizo - na unaweza kubadilishwa na maafisa wa afya ya umma.

Nini hufanyika iwapo WA Notify inaniambia kuwa huenda nimeambukizwa?

Iwapo WA Notify itagundua kuwa huenda umeambukizwa, taarifa kwenye simu yako itakupeleka kwenye wavuti ulio na maelezo kuhusu unachofaa kufanya. Hii inajumuisha jinsi na pahali pa kupimwa, maelezo kuhusu kujiweka salama na kuweka walio karibu nawe salama, na rasilimali za kujibu maswali yako. Ni muhimu kusoma na kufuata maelekezo kwenye wavuti kwa uangalifu.

Je, watu watajua iwapo nitapatikana na COVID-19?

La. WA Notify haishiriki maelezo yoyote kukuhusu na mtu yeyote mwingine. Mtu akipokea taarifa kuhusu mfiduo unaowezekana, wanajua tu kuwa mtu ambaye walikuwa karibu naye katika siku 14 zilizopita ameambukizwa COVID-19. Hawatajua mtu huyo au mahali aliambukizwa.

Je, nastahili kulipi WA Notify?

La. WA Notify ni ya bure.

Je, WA Notify itasaidia vipi jimbo la Washington?

Utafiti wa hivi karibuni wa University of Washington (Kiingereza pekee) ulipata kuwa watu wanavyozidi kutumia taarifa ya mfiduo, ndivyo manufaa yanakuwa makubwa. Matokeo yalionyesha kuwa WA Notify iliokoa karibu maisha 40 hadi 115 na huenda ikazuia karibu visa 5,500 vya COVID-19 wakati wa miezi minne ya kwanza ilipotumika. Mifumo ya data inaonyesha kuwa hata idadi ndogo ya watu wanaotumia WA Notify inaweza kupunguza maambukizo na vifo vya COVID-19, ikionyesha kuwa WA Notify ni zana bora ya kuzuia msambao wa COVID-19.

Je, WA Notify hufanya kazi nikisafiri nje ya jimbo?

Ndiyo. Ukisafiri kwenda jimbo lenye programu inayotumia teknolojia ya Apple/Google, simu yako itaendelea kubadilishana misimbo nasibu na watumiaji katika jimbo hilo. Hakuna haja ya kubadilisha chochote katika mipangilio ya programu yako. Ukitoja nje ya Washington kwa kipindi kirefu, unafaa kukagua chaguo katika jimbo lako jipya ili kupata usaidizi na arifa za ndani.

Kwa nini tunahitaji kufuatilia mwasilani na WA Notify?

Kufuatilia mwasilani kumekuwa uingiliaji faafu wa afya ya umma kwa miongo. WA Notify huauni kazi hii bila kujulikana. Huu ni mfano: Ukipatikana na COVID-19, maafisa wa afya ya umma wanaweza kukupigia na kukuomba kusambaza waasilani wako wa karibu wa hivi karibuni. Huwezi kumtaja mtu ambaye humjui lakini uliketi karibu naye kwenye basi. Iwapo nyinyi nyote wawili mna WA Notify, mtu huyo asiyejulikana kwenye basi anaweza kuarifiwa kuhusu mfiduo unaowezekana na kuchukua hatua za kuzuia msambao wa COVID-19 kwa marafiki na familia. Sawa tu na kunawa mikono na kuvaa barakoa husaidia kumaliza msambao wa COVID-19, pamoja ni faafu zaidi.

WA Notify huchukua muda upi kuwaarifu watumiaji wengine?

Watumiaji ambao huenda wameambukizwa COVID-19 na mtumiaji mwingine watapokea taarifa ndani ya saa 24 baada ya mtumiaji aliyeambikizwa COVID atafuata hatua katika WA Notify ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify bila kujulikana.

Je, inawezekana kupokea arifa anuwai kutoka kwa WA Notify?

Watumiaji ambao huenda wameambukizwa COVID-19 na mtumiaji mwingine watapokea taarifa ndani ya saa 24 baada ya mtumiaji aliyeambikizwa COVID atafuata hatua katika WA Notify ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify bila kujulikana.

Ni vipi naweza kuambia WA Notify iwapo nimeambukizwa COVID?

Iwapo umeambukizwa ugonjwa huo na afya ya umma imewasiliana nawe, watauliza iwapo unatumia WA Notify. Iwapo unatumia, watakutumia kiungo na/au taarifa ya uthibitishaji na kukusaidia kufuata hatua za kuiingiza kwenye WA Notify. Kiungo/taarifa hazijafunganishwa na maelezo yako ya kibinafsi. Afya ya umma haina njia yoyote ya kujua ni nani ataarifiwa na programu hiyo kuhusu mfiduo ukifuata hatua hizi. Taarifa hiyo ya mfiduo haitakuwa na maelezo yoyote kukuhusu. Watu wanaothibitisha matokeo yao bila kujulikana katika WA Notify wanavyozidi kushiriki misimbo yao, ndivyo tunaweza kuzuia bora msambao wa COVID-19.

Ikiwa umepatikana na maambukizo, na bado unahitaji kuthibitisha matokeo yako katika WA Notify, piga simu kupitia nambari ya simu ya COVID-19 kupitia 1-800-525-0127, kisha ubonyeze # na kufuata visituo vya WA Notify.

Je, kuna kitu nahitaji kufanya baada ya kuongeza WA Notify kwenye simu yangu?

Kitendo cha ziada kinahitajika tu iwapo:

 1. Utapatikana na COVID-19, au
 2. Utapokea taarifa kuwa huenda umeambukizwa.

Iwapo umeambukizwa ugonjwa huo, na afya ya umma imewasiliana nawe, watauliza iwapo unatumia WA Notify. Iwapo unatumia, watakutumia kiungo na/au taarifa ya uthibitishaji na kukusaidia kufuata hatua za kuiingiza kwenye WA Notify. Kiungo/taarifa hazijafunganishwa na maelezo yako ya kibinafsi. Afya ya umma haina njia yoyote ya kujua ni nani ataarifiwa na programu hiyo kuhusu mfiduo. Taarifa hiyo ya mfiduo haitakuwa na maelezo yoyote kukuhusu. Watu wanaothibitisha matokeo yao bila kujulikana katika WA Notify wanavyozidi kushiriki misimbo yao, ndivyo tunaweza kuzuia bora msambao wa COVID-19.

Iwapo WA Notify itagundua kuwa huenda umeambukizwa, taarifa kwenye simu yako itakupeleka kwenye wavuti ulio na maelezo kuhusu unachofaa kufanya. Hii inajumuisha jinsi na pahali pa kupimwa, maelezo kuhusu kujiweka salama na kuweka walio karibu nawe salama, na rasilimali za kujibu maswali yako. Ni muhimu kusoma na kufuata maelekezo kwenye wavuti kwa uangalifu. Taarifa haitakuwa na maelezo kuhusu mtu ambaye huenda amekuambukiza au ni wapi. Haijulikani kabisa.

Je, kutumia WA Notify kutamaliza betri yangu au kutumia data nyingi zaidi?

La. Imeundwa ili kuwa na athari ya chini kabisa kwenye data yako na maisha ya betri yako kwa kutumia teknolojia ya Bluetooth Low Energy technology.

Je, nahitaji kuwasha Bluetooth kila mara ili WA Notify iweze kufanya kazi?

Ndiyo. WA Notify inatumia Bluetooth Low Energy, hivyo lazima Bluetooth iwe amilifu ili mfumo uweze kuwagundua watumiaji wengine wa karibu.

Je, nahitaji kufungua WA Notify kwenye simu yangu ili iweze kufanya kazi?

La. WA Notify itafanya kazi katika mandhari nyuma.

Je, WA Notify huzuia vipi ripoti za kipimo cha uwongo?

WA Notify inawahitaji watumiaji kuthibitisha bila kujulikana vipimo chanya kwa kutumia kiungo au taarifa ya uthibitishaji uliotolewa na maafisa wa afya ya umma. Kiungo au taarifa haijafunganishwa na utambulisho wa mtu. Baada ya kubofya au kudonoa kiungo au taarifa ya uthibitishaji, WA Notify inaweza kulinganisha misimbo nasibu ya watumiaji ambao wamekuwa karibu na kuwaarifu kuhusu mfiduo unaowezekana. Taarifa haina maelezo yoyote kuhusu mtu ambaye huenda aliwaambukiza au ni wapi waliambukizwa.

Je, WA Notify inaauniwa kwenye simu janja mzee?

Watumiaji wa iPhone wanaweza kutumia WA Notify iwapo mfumo wako wa uendeshaji ni:

 • iOS toleo la 13.7 au la hivi karibuni (kwa iPhone 6s, 6s Plus, SE au mpya)
 • iOS toleo la 12.5 (kwa iPhone 6, 6 plus, 5s)

Watumiaji wa Android wanaweza kutumia WA Notify iwapo simu yako ya Android inatumia Nishati ya Chini ya Bluetooth na Android Toleo la 6 (API 23) au zaidi.

Je, ni lazima niwe na umri wa miaka 18 ili kutumia WA Notify?

La. WA Notify haijui wala kuangalia umri wako.

Je, teknolojia hii itafanya kazi nikishiriki simu na mtu mwingine?

WA Notify haiwezi kujua aliyekuwa akitumia simu wakati wa mfiduo. Iwapo mnashiriki simu, kila mtu anayetumia simu hiyo anahitaji kufuata maelekezo ya afya ya umma iwapo WA Notify itaonyesha kuwa huenda umeambukizwa COVID-19.

Je, WA Notify hufanya kazi katika vifaa kama iPad au saa janja?

La. Mfumo wa Taarifa ya Mfiduo ulisanidiwa hasa kwa simu janja na haifanyi kazi kwenye iPad.

Jimbo la Washington linafanya nini kutoa ufikiaji kwa teknolojia hii kwa watu ambao hawana simu janja?

WA Notify si zana pekee ya kusaidia kuzuia msambao wa COVID-19. Ufuatiliaji wa mwasilani na juhudi nyingine zinasaidia kila mkaaji wa Washington, hata kama hawana simu janja. Chanjo ni njia bora ya kukomesha msambao wa COVID-19, na kuvaa barakoa, kukaa mbali na wengine, na kupunguza ukubwa wa mikutano ni njia nyingine kila mtu anaweza kusaidia kukomesha msambao wa COVID-19.

Lifeline program (Mpango muhimu) wa serikali ya muungano unatoa mkopo wa bili ya simu kila mwezi kwa wanaofuzu. Baadhi ya watoaji huduma wa pasi waya wanaoshiriki wanaweza pia kutoa simu mahiri ya bila malipo. Jifunze mengi kuhusu mpango huo, anayefuzu, jinsi ya kutuma ombi na watoaji huduma wa pasi waya wanaoshiriki (Kiingereza pekee).

Kumbuka, kupata chanjo ya COVID-19 ndiyo njia bora ya kukomesha msambao wake.

Kwa nini inaonekana kama WA Notify inatumia betri zaidi?

Kwa kweli, haitumii. Utumiaji wa betri kwenye kifaa chako unaonyesha asilimia ya betri inayotumika kila siku inajumuisha programu kama WA Notify. Programu nyingi huwa haziendeshwi usiku. WA Notify pia haiendeshwi usiku, lakini HUWA inaangalia misimbo ya nasibu baada ya kila saa mbili kwa milingano ya mtumiaji mwenye maambukizo ili iweze kukuarifu kuhusu mfiduo wowote. Hivyo, kwa mfano, ikiwa hakuna programu nyingine ambazo zinaendeshwa wakati umelala, WA Notify itawakilisha asilimia ya juu ya betri iliyotumika wakati huo. Hiyo haimaanishi kuwa WA Notify inatumia betri nyingi - asilimia ya juu tu ya kiwango cha chini cha betri iliyotumika.

Washington ilitoa WA Notify katika zaidi ya lugha 30, kwa hivyo ni kwa nini naiona tu katika Kiingereza na Kihispania pekee kwenye duka la Google Play?

WA Notify hufanya kazi kutegemea lugha iliyowekwa kama chaguo msingi kwenye simu ya mtumiaji. Kuna toleo moja tu la WA Notify, lakini mizuko yoyote - taarifa ya mfiduo, kwa mfano - itaonekana kwa lugha ambayo mtumiaji anapendelea kati ya lugha zaidi ya 30 ambazo jimbo la Washington lilitekeleza.

Nilipokea taarifa na/au ujumbe wa matini lakini mtu aliyepimwa alikuwa mwanafamilia au mtu wa kaya. Nafaa kufanya nini?

Mtumiaji wa WA Notify aliyepatikana na maambukizo anafaa kuruhusu hatua za kuwaarifu wengine bila kujulikana ambao huenda wakaambukizwa, hivyo unafaa kupuuza ujumbe wowote au taarifa ambazo si zako.

Ikiwa mwanafamilia au kaya yako ni mtumiaji wa WA Notify, amepatikana na maambukizo, na bado anahitaji kuthibitisha matokeo yao katika WA Notify, wanaweza kupiga simu kupitia nambari ya simu ya COVID-19 kupitia 1-800-525-0127, kisha ubonyeze # na kufuata maagizo ya WA Notify. Simu ikijibiwa, ulizia kiungo cha uthibitishaji cha WA Notify.

Nina muda upi wa kudonoa taarifa au kuwezesha kiungo cha uthibitishaji?

Una saa 24 baada ya kupokea taarifa au ujumbe wa matini ili kufuata hatua za kuwaarifu wengine katika WA Notify. Ikiwa huwezi kudonoa taarifa au kubofya kiungo cha uthibitishaji ndani ya muda huo, tafadhali piga simu kupitia nambari ya simu ya COVID-19 kupitia 1-800-525-0127, kisha ubonyeze # na kufuata maagizo ya WA Notify. Simu ikijibiwa, ulizia kiungo cha uthibitishaji cha WA Notify. Unaweza pia kuomba kiungo ikiwa afya ya umma itawasiliana na wewe kuhusu matokeo yako ya COVID-19.

Kwa nini Washington ilichagua suluhisho hili?

Washington iliunda kikundi cha jimbo cha uangalizi, ikijumuisha wataalamu wa usalama na uhuru wa kiraia na wanachama wa jumuiya nyingi, ili kukagua suluhisho la Apple/Google. Kikundi hicho kilipendekeza ukubalifu utakaozingatia uaminifu wa jukwaa hilo, ulinzi wa data wa kiwango cha juu na matumizi ya majimbo mengine.

Nyenzo Zinazohusiana na Ajira na Biashara

Mafao ya Kukosa Ajira

Ikiwa umepoteza kazi, unaweza kustahiki mafao ya kukosa ajira. Ikiwa unahitaji maelezo kuhusu jinsi ya kujaza madai kwa ajili ya mafao ya kukosa ajira, unaweza kupiga simu 1-800-318-6022. Wakipokea simu, sema lugha yako ili kupata huduma za ukalimani.

Wafanyakazi na Wamiliki wa Biashara

Janga la virusi vya korona limeathiri mamia ya maelfu ya wafanyakazi na waajiri katika jimbo letu.

Ili kudumisha usalama wafanyakazi, waajiri wanapaswa:

 • Kuwaelimisha wafanyakazi wao kuhusu ishara na dalili za COVID-19 katika lugha ambayo wanaielewa.
 • Kutekeleza mpango wa kudumisha umbali wa kutengana.
 • Kufanya usafi na uuaji wa vimelea wa mara kwa mara.
 • Kuhakikisha unawaji wa mikono wa mara kwa mara na sahihi.
 • Hakikisha wafanyakazi wagonjwa wanakaa nyumbani.

Majibu kwa maswali ya kawaida kuhusu likizo inayolipwa ya ugonjwa, ufidiaji wa mfanyakazi na muhtasari wa masharti ya usalama wa mahali pa kazi zinapatikana kutoka Department of Labor & Industries (Idara ya Kazi na Viwanda) kwa lugha mbalimbali.

Ikiwa una wasiwasi juu ya usalama wa mahali pako pa kazi, unaweza kuwasilisha malalamiko kwa kuwapigia simu Department of Labor & Industries moja kwa moja kwa nambari 800-423-7233. Huduma za ukalimani kwa njia ya simu zinapatikana.

Ikiwa una maswali kuhusu biashara na wafanyakazi wako katika kipindi cha COVID19, unaweza kuwapigia simu Employment Security Department (Idara ya Usalama wa Wafanyakazi) kwa nambari 855-829-9243.

Nyezo za Huduma ya Afya na Bima ya Afya

Unaweza kustahiki bima ya afya ya bila malipo au ya gharama nafuu. Wapigie simu Health Care Authority (Mamlaka ya Huduma za Afya kwa nambari 1-855-923-4633. Wakipokea simu, sema lugha yako ili kupata huduma za ukalimani.

Bima ya Alien Emergency Medical (AEM) ni mpango kwa ajili ya watu ambao wanastahiki matibabu ya dharura ambazo hawakidhi vigezo vya uraia au uhamiaji, au ni mtu anayestahiki ambaye hajatimiza miaka 5 ya sheria.

Namba ya simu ya dharura ya Help Me Grow ya Washington 1-800-322-2588 inaweza kutambua mipango na huduma mbalimbali unazostahiki na kukusaidia kuziomba. Hii inajumuisha:

 • WIC (Mpango wa Afya wa Wanawake, Watoto wachanga & Watoto)
 • Bima ya Afya kwa watoto, wanawake wajawazito na watu wazima
 • Upangaji uzazi kupitia Mpango wa Take Charge
 • Kliniki za afya na upangaji uzazi
 • Vifaa vya ujauzito na mtoto mchanga
 • Usaidizi katika kunyonyesha
 • Pia wana mipango na nyenzo kuhusu vyakula.
Maelezo ya Wakimbizi na Wahamiaji

Office of Immigrant and Refugee Affairs (Afisi ya Mambo ya Wahamiaji na Wakimbizi) (OIRA) inawasaidia wahamiaji kuelewa maelezo muhimu kuhusu COVID-19 na kuhusu wasiwasi wa mhamiaji. Baadhi ya mambo mengine muhimu ya kuyafahamu:

 • Hospitali na kliniki haziruhusiwi kushiriki uraia au hadhi ya uhamiaji na ICE.
 • Kupimwa COVID-19 na kupata msaada au punguzo la huduma ya afya halitaathiri uwezo wako wa kuomba kadi ya kijani au uraia.
 • Unapaswa kuwa na nambari halali ya ustawi wa jamii kwa ajili ya mafao ya kukosa ajira. Ikiwa ungependa kuzungumza na mtu kuhusu namna ya kupata mafao ya kukosa ajira piga simu 1-800-318-6022.
 • Kupokea mafao ya kutokuwa na ajira hakutatishia uwezo wako wa kuomba au kadi ya kijani au uraia chini ya sheria ya Usaidizi kutoka kwa Fedha za Umma.
 • Unaweza kustahiki Likizo Yenye Malipo ya Familia na Matibabu katika Jimbo la Washington ili kumhudumia mtu ambaye anaugua Covid-19 au kujihudumia mwenyewe iwapo una virusi. Hupaswi kuwa nambari ya ustawi wa jamii ili kupata fao hili. ESD inakubali hati zingine za aina nyingi.
 • Iwapo unamiliki biashara na unatafuta usaidizi, hatua ya kutuma maombi ya mkopo kutoka kwa Federal Small Business Administration (Mamlaka ya Usaidizi wa Biashara Ndogo ya Nchi) haitaathiri uwezo wako wa kupata kadi ya mkaazi au uraia.

Office of Immigrant and Refugee Affairs (Afisi ya Mambo ya Wahamiaji na Wakimbizi) (OIRA) inapendekeza kuwa iwapo hauna uhakika kuhusu hali yako au ya mwanafamilia, au kuhusu manufaa yako, wasiliana na wakili wa uhamiaji, afisa wa uhamiaji au mwakilishi aliyeidhinishwa na Department of Justice (Idara ya Sheria) (DOJ). Unaweza kupata wakili kupitia American Immigration Lawyers Association (Shirika la Mawakili wa Uhamiaji la Marekani), au unaweza kutembelea tovuti ya shirika lililoidhinishwa na DOJ.

OIRA ina mipango ya kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji kwa ajili ya:

 • Utafutaji wa kazi na mafunzo.
 • Usaidizi katika uhamiaji.
 • Ushauri kwa vijana.
 • Msaada kwa wakimbizi wazee, watoto, wanafunzi na wengine.
 • Mipango ya kawaida ipo wazi kwa mbali katika kipindi cha COVID-19. Ofisi ina huduma mpya za kukusaidia kuomba kazi au mafao ya kukosa ajira, kusaidia elimu yako, na kutoa usaidizi wa makazi. Ustahiki katika Msaada wa Fedha za Wakimbizi na Msaada wa Matibabu wa Wakimbizi umeongezwa hadi Sept. 30, 2020.
 • Kwa huduma na maelezo zaidi, piga simu 360-890-0691.

Kwa maswali kuhusu haki za wahamiaji, kupata usaidizi wa rufaa kwa ndugu/marafiki ambao wamewekwa kizuizini, na maelezo mengine yanayohusiana, unaweza kuwasiliana na Mtandao wa Mshikamano wa Wahamiaji wa Washington (Washington Immigrant Solidarity Network) kwa nambari 1-844-724-3737. Huduma za ukalimani kwa njia ya simu unapatikana.

Afya ya Akili na Hisia

Huu unaweza kuwa muda mgumu sana. Ni kawaida wewe au uwapendao mnaweza kuhisi wasiwasi, huzuni, hofu au hasira. Hauko peke yako. Ni sawa kutafuta na kuomba msaada.

Kila mtu anaathiriwa tofauti msongo wa mawazo na hali ngumu. Kitu cha muhimu zaidi unachoweza kukifanya ni kujijali wewe mwenyewe, familia yako, na jamii vizuri kadri uwezavyo.

Je, ni nini kinakusaidia ili ukabiliane na nyakati za changamoto? Je, unaendelea kuwasiliana na kuingiliana na marafiki na familia? Labda unazingatia kupumua kwa nguvu na kujinyoosha, mazoezi kadhaa au usiku mzuri wa kulala? Kutenga muda kwa ajili ya kujijali ni kipaumbele, hata kama hupendelei, kunaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Wapigie simu Washington Listens kwa nambari 1-833-681-0211. Huduma za ukalimani kwa njia ya simu zinapatikana. Ili kukabiliana na janga la COVID-19, Washington imezindua mpango wa usaidizi unaoitwa Washington Listens. Watu wanaotumia huduma za Washington Listens wanapata usaidizi ili kuweza kudhibiti msongo wa juu wa mawazo na kukabiliana na mabadiliko kutokana na COVID-19. Washington Listens inapatikana kwa yeyote katika jimbo la Washington ili kuzungumza na mtaalam wa usaidizi. Mpiga simu anapata usaidizi na kuunganishwa na rasilimali za jamii katika eneo lake. Mpango unaficha utambulisho wa wanaohudumiwa.

Ikiwa upo kwenye mgogoro na unahitaji kuzungumza na mtu ili akupe unasihi, kuna machaguo machache.

 • Disaster Distress Helpline inatoa unasihi wa haraka wa mgogoro kwa watu wanaopitia matatizo ya kihisia yanayohusiana na majanga ya asili au yaliyosababishwa na binadamu Piga Simu 1-800-985-5990. Wakipokea simu, sema lugha yako ili kupata huduma ya ukalimani. Simu ya usaidizi inapatikana saa 24 kwa siku kila siku.
 • Crisis Connections ina Namba ya Simu ya Saa 24 ambayo inatoa usaidizi wa papo hapo kwa watu, familia na marafiki wa watu wenye tatizo la hisia. Inawahudumia watu wanaoishi Kaunti ya King. Huduma za ukalimani wa lugha zinapatikana. Piga simu 1-866-427-4747.
 • National Suicide Prevention Lifeline inatoa nyenzo za kinga na migogoro kwa watu wanaofikiria kuhusu kujiua. Wapendwa wako pia wanaweza kuwapigia simu lifelineili kupata rasilimali za kuisaidia familia na marafiki wao. Piga simu 1-800-273-8255. Namba ya simu hii inapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki. Kuna namba ya simu maalumu ya usaidizi kwa ajili ya wanajeshi wastaafu. Piga simu 1-800-273-8255 kisha bonyeza 1. Ikiwa wewe ni kipofu na una tatizo la kusikia, piga simu 1-800-799-4889.
Nyenzo za Vyakula

Ikiwa una mtoto mwenye umri wa miaka 18 au chini anaweza kupata chakula cha bure kutoka shule. Watu wazima wenye ulemavu waliojiunga katika mipango ya elimu pia wanaweza kustahiki chakula cha shule. Mara nyingi, milo hii hupelekwa au huwekwa katika maeneo ya nje ya shule kama vile vituo vya basi. Wasiliana na wilaya ya shule yako kufahamu kama wanatoa chakula cha bure.

Kwa wale wote wenye ujauzito, wamama wapya na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, unaweza kupata chakula kupitia mpango wa Department of Health’s Women, Infants and Children (WIC). Kwa usaidizi wa lugha, piga simu 1-866-632-9992.

Huenda hifadhi za chakula zimebadlisha saa za kazi au zinaweza kuwa zimefungwa kwa watu wanaotembelea maeneo yao kwa sababu ya ongezeko la mahitaji ya chakula katika kipindi cha Covid-19. Tafadhali piga simu kabla ya kwenda. Northwest Harvest ni mtandao wa hifadhi ya chakula ya jimbo zima. Andika jina la jiji lako kwenye kisanduku katika tovuti hii.

Ikiwa unaishi Mashariki ya Washington unaweza kupata orodha ya hifadhi za chakula katika Second Harvest. Chagua kaunti yako katika tovuti hii kwa ajili ya orodha ya hifadhi za chakula katika eneo lako.

Kadi za msaada wa vyakula vya msingi

Kadi za msaada vya vyakula vya msingi (EBT) zinaweza kununua vyakula na zinapatikana kwa watu mbalimbali. Raia wa Marekani wanaweza kuomba msaada huu katika ukurasa wa Vyakula vya Msingi kwenye tovuti ya Department of Social and Health Services (DSHS) ya Jimbo la Washington.

Kumbuka: Serikanli ya nchi ilisimamisha masharti ya kuwa na kazi ambayo yalitumika kwa baadhi ya watu wazima wakati wa mgogoro huu. Hata hivyo, serikali ya nchi inahitaji uwe raia wa Marekani ili uweze kustahiki kwa msaada huu.

Kadi zinazofanana na kadi za mkopo kama zilizoelezwa hapo juu zinapatikana kwa watu wengi ambao sio raia na ambao wanakidhi masharti yote mengine ya mpango. Unaweza kuomba msaada huu kupitia State Food Assistance Program wa DSHS (kwa Kiingereza pekee).

Maelezo na Rasilimali kwa Familia

Huu ni muda mgumu sana kwa familia nzima. Hizi hapa ni dondoo kadhaa za jinsi ya kuishughulikia hali hii pamoja na watoto wako:

Fanya majadiliano na familia katika sehemu nzuri na wahimize wanafamilia kuuliza maswali. Zingatia kuwa na mijadala tofauti na watoto wadogo ili kutumia lugha ambayo wanaweza kuielewa na kushughulikia hofu zao mahsusi au imani potofu.

Ingawa unapaswa kuendelea kupata taarifa, punguza kukaa kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii ambayo inaweza kuchochea woga na hofu. Kuwa na ufahamu hasa wa (na upunguze) kiasi cha taarifa za matukio katika vyombo vya habari au muda wa mitandao ya kijamii ambao watoto wako wanafuatilia kuhusu janga hili.

Zingatia kuwasaidia watoto kwa kuwahimiza waulize maswali na kuwasaidia kuelewa hali ya sasa.

 • Zungumza kuhusu hisia zao kisha uwaonyeshe unaelewa hisia zao.
 • Wasaidie kueleza hisia zao kupitia michoro au shughuli nzingine.
 • Fafanua taarifa potofu au kutoelewana kuhusu jinsi virusi vinaenea na kwamba si kila ugonjwa wa njia ya hewa ni virusi vipya vya korona ambavyo vinaweza kusababisha COVID-19.
 • Wapatie faraja na uvumilivu wa ziada.
 • Wakague watoto wako mara kwa mara au pale hali inapobadilika.
 • Weka ratiba ya familia yako inayofanana linapokuja suala la kulala, kula na mazoezi.
 • Tenga muda wa kufanya mambo nyumbani ambayo tatakufanya wewe pamoja na familia yako mjisikie vizuri katika hali zingine ngumu, kama vile kusoma, kutazama filamu, kusikiliza muziki, kucheza michezo, au kushiriki katika shughuli za kidini (maombi, kushiriki katika huduma Intaneti).
 • Tambua kwamba hisia kama vile upweke, uchovu, hofu ya kuambukizwa ugonjwa, wasiwasi, msongo wa mawazo, na hofu ni athari za kawaida katika hali gumu kama vile ya janga.
 • Isaidie familia yako kushiriki katika shuguli za burudani na muhimu zinazoendana na maadili ya familia na utamaduni wako.
Nyenzo na Maelezo ya Ziada

Washington State Commission on Asian Pacific American Affairs (CAPAA)